13 June 2012



Kanisa la Kianglikana la nchini Uingereza limepinga vikali mpango wa serikali wa kutaka kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Taarifa rasmi ya kanisa hilo imesema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa imeleta mgawanyiko na ni yenye mapungufu -na inayotishia kuleta Uhasama mkubwa baina ya Kanisa na Serikali.
Ikitoa jibu lake kuhusiana na swala hilo nchini Uingereza na Wales, kanisa imesema kuwa sheria hiyo haina uzito.
Mpango wa serikali kutaka kuruhusu ndoa za jinsia moja ifikapo mwaka 2015, huenda ikahujumu maadili ya kanisa la kitaifa. Hii ndio ilikuwa kauli ya kanisa.
Hata hivyo, taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani zimesema kuwa makanisa hayatashurutishwa kufungisha ndoa za jinsia moja na kwamba serikali itazingatia maoni kutoka pembe zote kabla ya kutunga sheria.
Nayo mashirika ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wametuhumu kanisa kwa kusambaza uvumi.
Kanisa linasema kuwa hatua yoyote ya kuruhusu ndoa kuwa kati ya wapenzi wa jinsia moja inakiuka maadili ya kanisa ambayo yamekuwa msingi wa kanisa kwa karne nyingi na ambao unasisitiza kuwa ndoa ni kati ya mke na mume wala sio vinginevyo. Aidha inasema kuwa kufanya hivyo itakuwa ni kuhujumu maana hii ya ndoa.

Mpenzi wa jinsia moja
Hatua ya Kanisa la England kuelezea wasiwasi kuhusu kutoweka kwa jukumu lake kubwa la kufungisha ndoa na kugusia uwezekano wa kupotoka kwa msingi wake , inalenga kutahadharisha umma juu ya ukubwa wa kile inachoamini ndio pendekezo la sheria kuhusu ndoa za jinsia moja.
Inasema kuwa taasisi kama hiyo yenye umuhimu kwa jamii kwa ujumla inahujumiwa ili kuafikia malengo ya kisiasa na inapendekezwa kwa maksudi kama kitu kilicho na umuhimu mkubwa.
Maafisa wa kanisa wametaja mashauriano yaliyofanyika kuhusiana na sheria hiyo kama yasiyo na uzito.
Kwa kanisa, ndoa ambayo lengo lake ni kupata watoto sio kitu ambacho wapenzi wa jinsia moja wanweza kupata. Kwa kuruhusu uchambuzi tofauti kuhusu maana ya ndoa inasisitiza kuwa mfumo wote utakuwa dhaifu kitu ambacho taifa hilo halistahili kuruhusu.
Maafisa wa kanisa wanadai ikiwa hoja yao ya kutotaka kufungisha ndoa za jinsia moja ingawa hawashurutishwi kufanya hivyo na sheria hiyo, itapelekwa katika mahakama za nyumbani na za nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya bila shaka watashindwa.
Waziri wa chama cha Tory Crispin Blunt , alisema kuwa hatua ya serikali kulinda makanisa dhidi ya kufungisha ndoa za jinsia moja huenda ikawa tatizo kisheria.
Lakini mapendekezo ambayo serikali inatoa ni kwamba ndoa inapaswa kuwa kati ya wapenzi wa jinsia moja au kati ya mwanamke na mwanaume.
Wakili wa haki za binadamu Lucy Scott-Moncrieff, na ambaye pia ni makamu rais wa chama cha wanasheria,
alisema kuwa mahakama ya muungano wa ulaya ina msimamo mzuri kuhusu maswala yanayoibua hisia tuauti za kidini.
Ikiwa swala hilo litapelekwa katika mahakama hiyo, majaji huenda wasikubali kwamba taasisi yoyote ya kidini itaweza kulazimishwa kufungisha ndoa za jinsia mojam, lakini akaongeza kuwa kun abaadhi ya makanisa ambayo yangependa kuruhusiwa kufungisha ndoa za jinsi moja.
BBC Swahili.


0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!